DR.MSOWOYA KUISHANGAZA IRINGA

Muimbaji wa nyimbo za injili Tanzania Dr. Tumaini Msowoya anatarajia kuishangaza Mafinga iliyopo mkoani Iringa mwishoni mwa mwaka huu. Akiongea hayo na mwandishi wetu, Dr. Msowoya alisema, anatarajia kuandaa tamasha kubwa alilolipa jina "Hakuna Matata Festival 2019". Katika tamasha hilo ambalo litaambatana na uzinduzi wa DVD ya Hakuna matata, litatanguliwa na semina kwa "Single mother" na "Single Father" kuangalia namna nzuri itakayowasaidia kuwalea watoto wao kimaadili, bila kukata tamaa na kuhakikisha wanatimiza ndoto zao kimaisha bila kufikiria wapo peke yao. Pia tamasha hilo litapambwa na waimbaji wa nyimbo za injili kutoka mikoa mbalimbali.

KIJANA ALIYEITEKA AFRIKA MASHARIKI

Godfrey Joseph Kapandila ni miongoni mwa washiriki wa Mashindano Makubwa ya Vipaji yanayokutanisha nchi zote za Afrika Mashariki yanayofahamika kwa jina la "East Africa Got Talent 2019" HISTORIA FUPI YA KIPAJI CHAKE. Godfrey Joseph Kapandila alijiunga na kituo cha Vijana cha Donbosco - Upanga mnamo mwaka 2009. Kituo hicho kipo chini ya usimamizi wa Shirika la Mapadre wa Donbosco ( The Salesian of Donbosco - SDB ) Kujiunga kwake ilikuwa ni kutokana na msukumo wa kaka zake ambao walikuwa wanajihusisha na masuala ya mziki katika kituo hicho. Godfrey alijiunga na kituo cha Donbosco na kuvutiwa sana na mchezo wa Basketball ijapokuwa alikuwa ni mwimbaji mzuri sana katika Shule ya Sekondari ya Jitegemee aliyokuwa anasoma. Mashindano makubwa ya mpira wa kikapu (Basketball) ambayo timu yao ilishiriki, yalimfanya Godfrey kuumia mguu hata kutokuwepo tena katika kikosi cha timu ya Basketball ya Vijana Donbosco. Ndoto zake zilihamia kwenye mziki, huko ndiko alipojifunza kupiga guitar na kuimba. Baadae alienda kujiendeleza kimziki na kuweza kumaliza vema masomo yake juu ya elimu ya mziki. Godfrey alitambua umuhimu wake ndani ya Kanisa kwani ndilo lililomlea na kuendeleza kipaji chake, hata hivyo alitumika vema ndani ya Kanisa katika makongamano mbalimbali ya TYCS, VIWAWA (Vijana Wakatoliki Wafanyakazi) pamoja na safari mbalimbali za Uinjilishaji zilizoandaliwa na Shirika la Donbosco ( The Salesian of Donbosco - SDB ) ndani na nje ya nchi akiwa kama mwimbaji na mpiga vyombo mbalimbali vya mziki. Aliposikia East Africa Got Talent 2019 imefika Tanzania alimuomba Mungu na kupiga moyo konde, alinyanyua nyayo zake na kukanyaga jukwaa la East Africa Got Talent 2019 kipaja kikubwa alichoonesha ni kutoa sauti ya kifaa cha mziki kiitwacho saxophone kwa kutumia mdomo na viganja vyake bila ya kutumia chombo halisia. Tulipomuhoji juu ya kipaji hicho, namna gani aliweza kuigundua sauti hiyo alisema: "ni Mungu tu ndiye amenijali kipaji hiki" Kipaji hiki sio cha kawaida katika East Africa Got Talent 2019 haikuwa rahisi Judges kuamini lakini umati wote ulijikuta ukipunga mikono juu, hata baada ya Godfrey Kapandila (Gsax) kupuliza #saxophone kwa mdomo wake akipiga wimbo wa "My heart will go on - Celine Dion" Judge Koinange Jeff alishindwa kujizuia na kumwambia; "You are the Human Saxophone". Mimi nawe tuungane kumuombea mafanikio.